NAMNA YA KUTENGENEZA CHAPATI
Unga kilo moja weka sukari kijiko kimoja cha chai pamoja na chumvi kijiko kimoja cha chai
weka mafuta ya kupikia yamoto kikombe kimoja cha chai kidogo kisha changanya
Kisha weka maji ya uvugu vugu kikombe kimoja cha chai kidogo na endelea kuchanganya
Kanda mpaka upate mchanganyiko mzuri laini na mkavu
Kata saizi ya unga ambao ukisukuma itatosha kwenye kikaango chako
huu
ni muonekano wa chapati ndogo itakayoweza kuenea katika kikaango kidogo
hata kwa matumizi ya nyumbani iweke kwenye kikaango cha moto bila
mafuta pika pande zote mbili
kisha weka mafuta naigeuze geuze
hii ni chapati yako imekamilika na ni laini na ina lea kama daftari na ni tamu kupita maelezo
TOA MAONI YAKO KAMA UNATAKA KUENDELEA POKEA MAFUNZO KWA NJIA YA
MY BLOG
Mail:arushaclan@gmail.com or Sms: +255 (0) 658859177