JINSI YA KUPIKA MGUU AU KIFUA CHA BATA
Kila
mmoja wetu anatambua ulaini na utamu wa nyama ya bata endapo utampika
vizuri. Fatilia hapo chini maelezo jinsi ya kukata vipande hivyo vya
nyama ya bata na jinsi ya kuitengeneza kwa mtindo safi kabisa, kama
ni kwenye mgahawa basi wateja wakula mlo huo watajitokeza kwa wingi na
kwa walaji wa nyumbani basi utakua umeongeza chaguo jingine katika
ratiba yako ya chakula, pika kifua cha bata acha watu wale kisha muulize
kila aliekula hii ni nyama gani utapata majibu mengi sana kuliko
utavyotegemea kwa sifa na ubora wa nyama hii.
Huyo ndio bata mzima akiwa ameshachinjwa na kusafishwa vizuri kabisa
Hivyo ni vifua vya bata kwa muonekano wa pande mbili mbele upande wa ngozi na nyuma sehemu yenye nyama tupu bila mfupa.
Huu ni mguu wa bata ukiwa na mfupa na haujatolewa ngozi kwa upande wa pili.
Vitu vta kuandaa ni
Kitunguu swaunu 1 kisage vizuri
Kitunguu maji 1 kata vidogodogo sana
Chumvi na pilipili manga
Maji 100gr
Juisi ya chungwa 1
Asali ya nyuki vijiko 4 vikubwa vya chakula
Bay leaf 1
Oregano kijiko nusu kidogo
Rosemary kijiko nusu kidogo
Mafuta ya maji yakupikia 150ml
Zabibu kavu 150 gr
Kama
inavyoonysha katika mtiririko wa kuandaa vitu vya kupika pamoja na bata
wako nimesema mafuta ya maji ya kupikia tumia yeyote kulingana na uwezo
wako
Chukua vitu vyote ulivyoandaa hapo juu weka katika bakuli kama unavyoona katika picha changanya kwa pamoja vyote.
Kisha
weka nyama kwenye chocmbo kitakachotosha vizuri halafu mwagia juu ya
nyama ya bata mbichi ule mchanganyiko wako safi usambaze kote.
Weka
nyama yako ndani ya friji lenye nyuzi joto 4 hadi 5 kwa masaa mawili
kuruhusu ule mchanganyiko wako uingie vizuri katika nyama.
kama
hauna friji usiweke kwenye friza acha nje sehemu yenye hewa safi na sio
joto kwa muda wa saa 1 ukiwa umefunika ili wadudu wasiingie.
Baada
ya muda huo kupita chukua nyama yako ya bata weka katika kikaango
chenye mafuta kiasi na moto wa wastani kaanga pande zote mbili pole pole
na nyama itaiva vizuri sana ikiwa na ladha safi.
Ule
mchanganyiko wako wa mwanzo wa viungo uliomuunga bata wako kabla ya
kupika usitupe hifadhi pembeni kwajili ya kutengeneza mchuzi wa kula
pamoja na nyama hiyo ya bata.
Kwa
wale wasio penda mafuta unaweza choma nyama hiyo katika jiko la mkaa
lenye moto wa wastani ili nyama hii iive taratibu isibabuke kama
unavyoona hapo chini katika picha.
Hapo
chini ni muonekano wa nyama ya bata ikiwa imeshaiva na kukatwa slice za
wastani bila kuachanisha kifua hicho ili kisipoteze muonekano wake
halisi.
Hapo chini ni muonekano wa ule mchanganyiko uliotumia kumuunga bata akiwa mbichi kabla ya kumpika.
Chukua
mchanganyiko huo wote weka katika sufuria au kikaango, washia jiko moto
wa wastani ili mchuzi huo uive pole pole pia ongezea na glass moja ya
mvinyo mwekundu au ( Redwine).
Hapo chini ni chupa na kipimo ambacho ni glasi halisi ya wine
Red
wine italeta harufu na ladha nzuri sana kwa wale wasiotumia pombe wawe
na amani kwani pombe yote inabadilika kua mvuke na kuisha kabisa
kinachobaki ni harufu nzuri na ladha ya zabibu iliyovundikwa.
Acha ichemke pole pole mpaka itakua nzito kutokana na sukari iliyopo kwenyemaji ya machungwa na zabibu kavu.
Ikishakua nzito tafadhali toa katika jiko tayari kwa kusave sauce hii
unamwagia juu ya bata au unaweka katika chombo kidogo unasave pamoja na
nyama hiyo ya bata mlaji atajipimia kiasi cha sauce anachopenda.
Muonekano wa upangaji sahani hapo chini hii yote ni kumvutia zaidi mlaji na kukifanya chakula chako kionekane safi na salama.
Nyama
hii ya bata unaweza savu na ugali, wali, viazi hata mihogo ya kuchemsha
vyovyote upendavyo na utafurahia zaidi ikiwa umefata maelezo vizuri ya
uandaaji.
Naimani
mtakua mmefurahia sana mapishi haya ya nyama ya Bata. Ukifatilia toka
mwanzo nimekua nagusia vyakula ambavyo watu wengi hawapendi sana kula
aidha kwakukosa umaarufu au kwa kutokufahamu njia mbada ya kukipika ili
kipendeze na kiweze kulika.
Tengeneza
bata huyu na usimueleze mlaji kisha baada ya mlaji kula muulize anahisi
nyama hii ni nyama gani? kuanzia hapo yule asiye mpenzi wa kula bata
atakua mwanachama mzuri sana mama nyumbani unakua umeongeza idadi ya
mabadiliko ya chakula nyumbani.
Kuna
mdau alieuliza oregano ni nini? hapo chini ni picha ya spice inayoitwa
oregano zinapatikana sana kila duka la chakula hapo nyumbani Tanzania na
uliza kwa jina hilo hilo supermaket yeyote ile utapata natumai utakua
umeifahamu na kwenda kuinunua na ni nafuu bei yake.
Mdau
ulie uliza mbadala wa Redwine kwaruza ganda la limao au chungwa upate
zile chenga chenga kijiko kimoja cha chai then weka katika mchanganyiko
wako utapata harufu safi na ladha nzuri sana.
TOA MAONI YAKO KAMA UNATAKA KUENDELEA POKEA MAFUNZO KWA NJIA YA
MY BLOG
Mail:arushaclan@gmail.com or Sms: 0658859177